Kutokana na serikali kufanya mabadiliko ya mihula mwaka wa masomo 2022 ili kupisha zoezi la sensa. Ambapo muhula wa kwanza unaisha mwezi Julai tarehe 28 na muhula wa pili kuanza Septemba 5, 2022.
Kwa barua hii napenda kukujulisha kuwa mabadiliko hayo ya mihula ya masomo hayaathiri wala kubadidli awamu za ulipaji ada na muda wa malipo.
Hivyo basi awamu ya tatu ya malipo ya ada itaanza Julai 1 na awamu ya nne itaanza Oktoba 1 (Hii ni kwa madarasa yasiyo ya mtihani)
Kwa madarasa ya mitihani (darasa la nne na la saba) awamu ya tatu na ya mwisho itaanza Julai 1 lengo la kufanya hivi ni kufanikisha uendeshaji wa shughuli za kila siku za shule.
Aidha tumeambatanisha na kipeperushi cha ratiba za mihula ya malipo ya ada ili kukumbusha awamu na kiasi cha malipo.
Tafadhali lipia kupitia akaunti ifuatayo:- 0150316711000 benki ya CRDB tawi lolote au Fahari huduma hapa shuleni kwetu.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba 0786121813 – MWL MKUU au
0754 071973 – MKURUGENZI
Wako katika malezi.
……………………………………..
MANKUNGA HUSSEIN
( MKUU WA SHULE)