Ratiba ya Matukio Muhimu Kuelekea Mwisho wa Mwaka wa Shule
Tunapokaribia kufunga mwaka wa masomo, tungependa kuwajulisha wazazi, wanafunzi, na wadau wote kuhusu matukio muhimu yatakayofanyika katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba. Haya ni matukio ya umuhimu wa kipekee kwa maendeleo ya wanafunzi wetu na mipango ya shule kwa mwaka ujao.
Tafadhali zingatia ratiba ifuatayo:
Tukio | Tarehe |
---|---|
Mtihani wa Taifa Darasa la Nne | 23 – 24 Oktoba 2024 |
Mtihani wa Taifa Kidato cha Pili | 28 Oktoba – 5 Novemba 2024 |
Mtihani wa Kufunga Muhula wa Pili | 20 – 27 Novemba 2024 |
Safari ya Beach na Wanafunzi Wote | 29 Novemba 2024 |
Usaili wa Wanafunzi Mwaka 2025 | 30 Novemba 2024 |
Siku ya Wazazi | 7 Desemba 2024 |
Tunawaomba wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wamejiandaa kikamilifu kwa kila tukio, na wanashiriki kwa wakati. Matukio haya ni sehemu muhimu ya kujenga msingi wa masomo na malezi ya wanafunzi wetu.
Asanteni kwa ushirikiano wenu.
Uongozi wa Shule